Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 00:38

Tanzania yakanusha rais kuzawadiwa na Kempiski


Rais Jakaya Kikwete aakipiga akura yake katika kijiji chake huko Msoga octoba 31, 2010

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania anasema habari hizo hazina ukweli hata kidogo

Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ya Ikulu jijini Dar es salaam nchini Tanzania imekanusha habari zilizosambaa hivi sasa kupitia mtandao wa wiki leaks zikimuhusisha rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na zawadi zinazodaiwa kutolewa kwake na mmiliki wa hoteli ya zamani Kilimanjaro Kempistki Bwana Ally Algwadi.

Habari hizo zinadai kuwa Rais Kikwete wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na mgombea urais mwaka 2005 alisafirishwa kwenda London, Uingereza na kununuliwa suti tano pamoja na chama chake cha mapinduzi- CCM kupatiwa kiasi cha dola milioni moja za kimarekani kwa ajili ya kusaidia kampeni za chama chake ambavyo vyote vinadaiwa kutolewa na bwana Algwadi ambaye ni raia wa falme za kiarabu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Salva Rweyemamu taarifa hizo zinazodaiwa kutolewa na aliyewahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzani hazina ukweli bali zinalenga kumdhalilisha Rais na Tanzania kwa ujumla.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kulingana na kumbukumbu zilizopo Rais Kikwete hakuwahi kusafiri kwenda London katika kipindi kinachotajwa au kuhusika na uchangishaji na ukusanyaji wa fedha wakati wa kampeni zake.

Amesema si kazi ya mgombea kuchangisha pesa wakati wa kampeni lakini alipochaguliwa kuwa Rais alipelekewa orodha ya watu waliochangia katika kampeni na wala hoteli hiyo ya Kilimanjaro kempiski haikuwemo.

XS
SM
MD
LG