Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:47

Rais wa Sri Lanka aondoka nchini kufuatia shinikizo la waandamanaji


Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa, wakati wa maadhimisho ya uhuru wa taifa mjini Colombo, Feb 4, 2022. Picha ya AP
Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa, wakati wa maadhimisho ya uhuru wa taifa mjini Colombo, Feb 4, 2022. Picha ya AP

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameondoka nchini mapema Jumatano kuelekea kisiwa jirani cha Maldives, maafisa wamesema.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73, mke wake na mlinzi wake ni miongoni mwa abiria wanne waliokuwa ndani ya ndege ya kijeshi ya Sri Lanka aina ya Antonov 32 ambayo iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Colombo, maafisa wa idara ya uhamiaji wameiambia AFP.

“Hati zao za kusafiria ziligongwa muhuri na wakapanda ndege maalum ya jeshi la anga,” afisa wa idara ya uhamiaji aliyehusika katika mchakato huo amesema.

Haikuthibitishwa mara moja kwamba Rajapaksa amefika Maldives.

Maafisa wa uwanja wa ndege wamesema ndege hiyo ilizuiliwa kwa zaidi ya saa moja kwenye uwanja bila kuweza kupaa kufuatia mkanganyiko juu ya kibali cha kuruhusiwa kutua Maldives.

“Kulikuwa hali ya kutatanisha, lakini mwishowe kila kitu kilikwenda vizuri,” afisa wa uwanja wa ndege amesema, kwa sharti la kutotajwa jina.

Ameongeza kuwa wengi kati ya watu wa karibu na rais hawakusafiri naye ndani ya ndege hiyo.

Awali, Rajapaksa aliahidi kutangaza kujiuzulu kwake leo Jumatano, akisema anataka kuruhusu “utawala wa mpito kwa njia ya amani.”

XS
SM
MD
LG