Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 18:31

Rais wa Sri-Lanka amejiuzulu akiwa uhamishoni


Waandamanaji wakiwa katika ikulu ya rais nchini Sri-Lanka July 13 2022 PICHA: AP

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaska amejiuzulu akiwa Singapore.

Hali ya utulivu imeanza kurejea katika mji mkuu wa Colombo, Sri Lanka.

Amri ya watu kutotoka majumbani mwao imetangazwa na maafisa wa jeshi wameshika doria kote mjini humo ili kuzuia kutokea kwa ghasia.

Rajapaksa, alikimbilia Maldives jumatano wiki hii baada ya waandamanaji kuvamia ikulu ya rais, amewasili Singapore hii leo.

Maandamano yanatokana na hali mbaya ya uchumi.

Hatua ya r ais Rajapaska kumtangaza waziri wake mkuu Ranil Wickremesinghe kuwa kaimu rais, ilisababisha maandamano makubwa na kupelekea waandamanaji kuvamia bunge Pamoja na ofisi ya waziri mkuu wakimtaka aondoke madarakani.

Kundi dogo la waandamanaji wamekusanyika nje ya ofisi ya rais mjini Colombo huku waandaaji wa maandamano hayo ya kupinga serikali wakisema kwamba wataendelea na maandamano hadi utawala bora utakapopatikana.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG