Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:48

Rais wa Somalia asema kuwa operesheni dhidi ya al-Shabab itaendelea hadi ushindi upatikane


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza akiwa Pentagon, June 21, 2023,

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, Jumanne amesema kwamba operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabab itaendelea hadi pale ushindi utakapopatikana.

Mohamud ameyasema hayo siku moja baada ya vikosi vya serikali kuondoka kwenye miji kadhaa kufuatia mashambulizi mabaya yaliyotekelezwa na al Shabab dhidi ya wanajeshi kwenye kijiji cha Cowsweyne hapo Jumamosi.

Kiongozi huyo amesifu wanajeshi wa serikali walioondoa wanamgambo kutoka ngome zao tangu kuanza kwa operesheni mwaka jana, huku akiwashukuru wanajeshi pamoja na wapiganaji walioshirikiana nao.

Rais huyo amekanusha madai ya al-Shabab kwamba wanajeshi 178 waliuwawa kwenye shambulizi la Cowsweyne. Badala yake amesema kwamba al-Shabab walipoteza zaidi wakati wafu wao wakizikwa kwenye makaburi ya halaiki. Ameongeza kwamba kundi hilo lilipoteza wapiganaji 190.

Forum

XS
SM
MD
LG