Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:15

Rais wa Somalia anusurika kuuwawa


Rais wa Somalia Sharif Sheikh Sharif Ahmed(C) ambaye amenusurika kuuwawa akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Matt Baugh (R) balozi wa Uingereza nchini Somalia

Kundi la al-Shabab limeshindwa jaribio lake la kutaka kumuuwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed amenusurika kutokana na jaribio la kuuwawa lililopangwa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Watu wenye silaha walifyatua risasi kwenye msafara wa Rais hapo Jumanne katika eneo la Alamanda, kusini ya Somalia. Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika aliyekuwa kwenye msafara huo wa magari anasema Rais hakujeruhiwa lakini mlinzi mmoja aliuwawa na watu saba wengine walijeruhiwa.

Maafisa nchini Somalia wanasema wamewakamata watu wane kati ya washukiwa washambuliaji. Al-Shabab walidai kuhusika na shambulizi hilo kupitia tovuti yao.

Rais alikuwa akirudi kwenye mji mkuu Mogadishu baada ya kuutembelea mji wa Afgoye. Majeshi ya Umoja wa Afrika nay a serikali ya Somalia yalichukua udhibiti wa mji huo kutoka kwa kundi la al-Shabab wiki iliyopita.


XS
SM
MD
LG