Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 01:32

Rais wa Senegal Macky Sall kufanya ziara Russia na Ukraine kwa niaba ya AU


Rais wa Senegal Macky Sall akimkaribisha Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwenye Ikulu mjini Dakar, May 22, 2022. Picha ya Reuters.

Rais wa Senegal Macky Sall Jumapili amesema atafanya ziara siku za hivi karibuni nchini Russia na huko Ukraine kwa niaba ya Umoja wa Afrika, kama kiongozi wa Umoja huo.

Ziara hiyo ilikuwa ifanyike tarehe 18 Mei lakini haikuwezekana kutokana na masuala ya ratiba na tarehe mpya zimepangwa, Sall amesema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anayefanya ziara nchini Senegal.

Alipewa mamlaka na Umoja wa Afrika kufanya ziara hiyo, na Russia ilitoa mwaliko, ameongeza.

“Mara tu mambo yatakuwa yamekamilika, nitaenda bila shaka Moscow na pia Kyiv na tumekubaliana kuwashirikisha viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika ambao wanataka kuzungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye alielezea nia yake ya kuwasaliana na viongozi wa nchi za Afrika,” Sall amesema, akiongeza kuwa hilo pia litafanyika katika wiki zijazo.

Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine ambao umeathiri vibaya uchumi wa Afrika kutokana na kupanda kwa bei ya nafaka na uhaba wa mafuta, umeonyesha mgawanyiko kati ya nchi za Afrika kuhusu namna ya kutatua mzozo huo.

Mapema mwezi Machi, Senegal ilijizuia kupiga kura ya kuidhinisha azimio la Umoja wa mataifa lililopitishwa kwa kura nyingi, ambalo lilitoa wito kwa Russia kuondoka nchini Ukraine.

Hata hivyo, wiki chache baadaye, Senegal ilipigia kura azimio jingine lililoitaka Russia kusitisha vita.

Karibu nusu ya nchi za Afrika zilijizuia kupiga kura au hazikupiga kura kabisa katika maazimio hayo mawili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG