Mswaada huo ambao shirika la habari la Reuters umeuona unapendekeza kufanyika kwa uchaguzi wa bunge na rais Oktoba mwaka huu,na kisha waliochaguliwa wachukue madaraka hapo Desemba, wakati wakihudumu kwa muhula wa miaka mitano hadi 2028.
Taifa hilo kwa kipindi cha wiki 8 limeshuhudia maandamano makali dhidi ya serikali yaliyopelekea vifo vya takriban watu 48, wakati wa mapambano kati yao na maafisa wa usalama, na hasa kwenye maeneo ya kusini yenye utajiri mkubwa wa madini ya shaba.
Waandamanaji wamekuwa wakidai uchaguzi wa haraka uitishwe baada ya rais wa mrengo wa kushoto Pedro Castillo kuondolewa madarakani Desemba mwaka uliopita. Waziri mkuu Aberto Otarola anatarajiwa kuwasilisha mswaada huo kwenye tume maalum ya bunge baadaye Ijumaa. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mapendekezo kadhaa ya kuitisha uchaguzi kufeli mbele ya bunge.
Facebook Forum