Kwa mujibu wa msemaji wa Mamlaka za Palestina Nabil Abu Rudeine ni kwamba uamuzi wa Abbass kurejea Ramallah unakuja baada ya dakika chache kufuatia shambulio la Israel kuilenga hospitali ya Al Ahli katika mji wa Gaza na kusababisha vifo visivyopungua 900 na idadi kubwa ya majeruhi waliokuwa wakitibiwa kutokana na athari za mashambulizi ya Israel katika maeneo tofauti ya ukanda wa Gaza.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas achukua uamuzi wa kutoshiriki kwenye mkutano wa kilele siku ya Jumatano mjini Amman, mkutano unaowajumuisha viongozi wanne akiwemo rais Abdel Fattah el-Sissi wa Misri, rais Joe Biden wa Marekani na Mfalme Abdullah wa Jordan ili kujadili mzozo wa Israel na Palestina.
Forum