Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 21:17

Rais wa Nigeria atoa wito kumaliza ghasia


Rais wa nigeria Goodluck Jonathan akipongezwa na baadhi ya viongozi baada ya kuchaguliwa kuwa rais

Rais wa nigeria Goodluck Jonathan ametoa wito wa kumaliza ghasia upande wa kaskazini wenye waislamu wengi. Wafuasi wa upinzani wamezusha ghasia kupinga matokeo ya uchaguzi. Watu wengi inasemekana wameuawa katika ghasia hizo.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametoa mwito wa kumaliza ghasia kaskazini mwa nchi hiyo ambako kuna waislamu wengi kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa rais.

Katika hotuba yake Jumatatu jioni bwana Jonathan alisihi kuwepo umoja wa kitaifa akisema kuwa hakuna ushawishi wa kisiasa wa mtu yoyote ulio na thamani kuliko damu ya raia wa Nigeria yoyote.

Shirika la msalaba mwekundu limesema watu wengi wamekufa na maelfu kukoseshwa makazi Jumatatu wakati ghasia zilipozuka upande wa kaskazini kupinga matokeo ya uchaguzi.

Wafuasi wa upinzani wanadai kuwa kura ziliibiwa na wamechoma moto nyumba, matairi pamoja na kurushia mawe polisi.

Bwana Jonathani amepata kura nyingi kati ya asilimia 57 zilizohesabiwa hivyo kuepuka uchaguzi wa marudio.

Hakuna chama chochote cha upinzani kilichotia saini katika matokeo ya mwisho .

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG