Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 01:53

Rais Jonathan wa NIgeria huwenda akabaki madarakani


Kiongozi wa zamani wa Kigeni mgombea mkuu wa Upinzani akipunga mkono baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Daura, Nigeria April 16, 2011.

Tovuti ya tume huru ya uchaguzi ya Nigeria inaonyesha Bw.Jonathan akiwa ameshinda majimbo 21 kati ya 29.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amechukua uongozi mkubwa katika matokeo ya awali ya urais wakati hesabu ya kura ikiendelea huko katika taifa hilo lililo na idadi kubwa ya watu Afrika.

Tovuti ya tume huru ya uchaguzi ya Nigeria inaonyessha Bw.Jonathan akiwa ameshinda majimbo 21 kati ya 29 ambayo matokeo yametolewa.

Mpinzani mkuu Muhamad Buhari amepata kura nyingi katika majimbo ya kaskazini anakotokea ambako kuna waislam wengi.

Ili kushinda na kuepuka uchaguzi wa duru ya pili mgombea anahitaji kupata wingi wa kura na walau robo ya kura katika majimbo 24 kati ya 36 ya nchi hiyo.

Polisi walisema bomu moja lilipuka jumamosi usiku katika hoteli moja huko kaskazini mwa Nigeria na kujeruhi watu 8.

Sababu ya mlipuko huo haijulikani na bomu hilo lilipuka huko Kaduna nyumbani kwa makamu rais Namadi Sambo.

XS
SM
MD
LG