Upatikanaji viungo

Obama ataelezea mkakati wa kupambana na ISIS Iraq


Rais wa Marekani Barack Obama

Rais wa marekani Barack Obama ataelezea mkakati wake wa kupambana na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State huko Irak na Syria katika hotuba kwenye televisheni Jumatano usiku.

Msemaji wa ikulu ya marekani Josh Earnest amesema bwana Obama anaamini kuwa hiki ni kipaumbele kikubwa cha usalama wa nchi.

Amesema rais atazungumzia kuhusu kitisho kinachotolewa na wanamgambo wa Islamic State na mpango wake wa kulidhalilisha na kulivunja kundi la Islamic State.

Ernest hajafafanua kitu alichopanga bwana Obama kuzungumzia, lakini rais Obama tayari amefuta uwezekano wa kurejesha majeshi ya Marekani nchini Iraq.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG