Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 14:16

Rais wa Malawi azindua mradi wa kitaifa wa kuimarisha kilimo


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera alipokuwa ametembelea Washington Sep 28, 2022
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera alipokuwa ametembelea Washington Sep 28, 2022

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amezindua mradi wa kilimo kwa jina “mega farms”, unaolenga kuimarisha uchumi wa kilimo wa taifa hilo, pamoja na kumaliza uhaba wa chakula unaoshuhudiwa mara kwa mara.

Kila mwaka Malawi imekuwa ikishuhudia uhaba wa chakula licha ya juhudi nyingi za kuongeza uzalishaji ikiwepo program ya Targeted Inputs, inayotoa mbegu na mbolea za bei nafuu kwa wakulima.

Kulingana na ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na mtandao unaotahatharisha kuhusu kiangazi wa Famine Early Warning Systems Network, takriban watu milioni 4.4 wa Malawi ambao ni sawa na asilimia 22 ya jumla ya wakazi nchini humo, wanakumbwa na uhaba wa chakula, wakati hali hiyo ikitarajiwa kuongezeka kuanzia Oktoba mwaka ujao.

Akizungumza kwa njia ya televisheni wakati wa uzinduzi wa mradi huo mpya, Chakwera amesema kwamba unalenga kuongeza fedha za kigeni nchini, pamoja na kuhakikisha kujikimu kichakula.

Forum

XS
SM
MD
LG