Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 12:29

Rais wa Liberia akubali kushindwa na mpinzani wake Joseph Boakai


Rais wa Liberia George Weah (L) akiwa na mpinzani wake Joseph Boakai. November 13, 2023
Rais wa Liberia George Weah (L) akiwa na mpinzani wake Joseph Boakai. November 13, 2023

Maafisa wa uchaguzi wamesema asilimia 99.58 ya kura zimehesabiwa kutoka uchaguzi wa Jumanne, Boakai alikuwa akiongoza akiwa na asilimia 50.89  na Weah akiwa na asilimia 49.11 ya kura. Matokeo yalikuwa ni mabadiliko kwa miaka sita iliyopita wakati Weah alipomshinda kirahisi Boakai katika duru ya pili

Rais wa Liberia George Weah amekiri kushindwa Ijumaa jioni baada ya matokeo ya awali ya duru ya pili ya upigaji kuonyesha kuwa mpinzani wake Joseph Boakai amemshinda kwa pointi ya idadi ndogo ya kura.

Maafisa wa uchaguzi wamesema kwamba asilimia 99.58 ya kura zimehesabiwa kutoka uchaguzi wa Jumanne, Boakai alikuwa akiongoza, akiwa na asilimia 50.89 na Weah akiwa na asilimia 49.11 ya kura. Matokeo yalikuwa ni mabadiliko kwa yale ambayo yalikuwa miaka sita iliyopita wakati Weah alipomshinda kirahisi Boakai katika duru ya pili.

“Watu wa Liberia wamezungumza, na tumesikia sauti zao,: Weah alisema katika hotuba yake kwa taifa, akiongezea kuwa Boakai, “anaongoza kile ambacho sisi tumeshindwa kukivuka.”

Hotuba ya kukubali kushindwa ilitolewa kabla ya matokeo rasmi kutangazwa nchini Liberia na imekuja wakati ambako kumekuwepo na ongezeko la wasi wasi kuhusu kushuka kwa demokrasia Afrika Magharibi. Eneo hilo limeshuhudia wimbi la mapinduzi katika muda wa miaka kadhaa iliyopita, ikiwemo mwaka mapema mwaka huu yale yaliyotokea nchini Gabon baada ya uchaguzi wa rais.

Weah amesema alikuwa na “heshima kubwa kwa mchakato wa demokrasia ambao umelionyesha taifa letu.”

Mwanasoka wa zamani wa kimataifa mwenye umri wa miaka 57 alishindwa uchaguzi mwaka 2017 baada ya kutoa ahadi ya kupambana na umaskini na kuboresha maendeleo ya miundo mbinu. Ilikuwa ni makabidhiano ya kwanza ya kidemokrasia ya madaraka katika taifa hilo la Afrika Magharibi tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati yam waka 1989 na 2003 ambavyo vimeua takriban watu 250,000.

Lakini Weah amekuwa akishutumiwa kwa kutotimiza ahadi zake za kampeni ambazo alisema atapambana na rushwa na kuhakikisha haki kwa waathirika wa vita.

Boakai mwenye umri wa miaka 78, alihudumu kama makamu wa rais chini ya utawala wa Ellen Johnson Sirleaf, kiongozi wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa kidemokrasia. Alionekana kuwa na fursa nzuri katika upigaji kura kwasababu wananchi wengi wa Liberia wamekatishwa tamaa na kutotimizwa kwa ahadi za Weah kurekebisha uchumi mbaya wa nchi na kuondoa rushwa, amesema Ryan Cummings, mkurugenzi wa taasisiya ushauri ya Signal Risk kwa Afrika.

Matokeo ya duru ya pili hadi sasa yanaonyesha, “kutoridhishwa kwa umma na utawala wa Weah huku Boakai akionekana kuwa ni mbadala mzuri kwa waliberia wengi, “amesema Cummings.

Weah ni muafrika pekee aliyeshinda tuzo ya soka ya kimataifa ya Ballon d”Or. Alichea kama fowadi kwa timu ya Paris Saint-Germain, AC Milan, Chelsea na Manchester City katika miaka yake 18 ya uchezaji soka. Mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23, Tim, hivi sasa anacheza katika klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG