Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:30

Rais wa Kazakhstan ameidhinisha vikosi vya usalama kupiga risasi na kuua bila onyo


Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev akizungumza kwenye televisheni. January 5, 2022.
Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev akizungumza kwenye televisheni. January 5, 2022.

Rais Kassym-Jomart Tokayev alisema ni ujinga kushauriana na waandamanaji ambao aliwaelezea kama waalifu na wauaji.

Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev alisema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni leo Ijumaa kwamba ameidhinisha vikosi vya usalama vya nchi hiyo “kupiga risasi na kuua bila onyo” wakati akijaribu kumaliza maandamano dhidi ya serikali. Rais Kassym-Jomart Tokayev alisema ni ujinga kushauriana na waandamanaji ambao aliwaelezea kama waalifu na wauaji.

Kiongozi huyo wa Kazakhstan alisema wanajeshi wa kulinda amani wa Russia walikuwa nchini humo kwa kwa muda kufuatia ombi lake ili kuhakikisha usalama. Mapema Ijumaa, Tokayev alisema katika taarifa kwamba utaratibu wa kikatiba kwa kiasi kikubwa umerejeshwa baada ya machafuko ya wiki moja katika nchi hiyo ya Asia ya kati.

Serikali za mitaa zinadhibiti hali hiyo. Lakini magaidi bado wanatumia silaha na kuharibu mali za raia. Kwa hivyo hatua za kukabiliana na ugaidi zinapaswa kuendelezwa hadi wanamgambo waangamizwe kabisa, ilisema taarifa ya rais. Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba milio ya risasi bado ilisikika Ijumaa asubuhi huko Almaty jiji kubwa zaidi la nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG