Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 04:52

Rais wa Ivory Coast atangaza baraza jipya la mawaziri


Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara

Mabadiliko katika serikali ya Alassane Ouattara huenda ikawa hatua mojawapo ya kujiandaa na uchaguzi wa rais mwaka 2020, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara ametangaza baraza jipya la mawaziri Jumatano ambapo Adama Coulibaly anabaki katika nafasi yake ya Waziri wa Fedha, kulingana na taarifa ya serikali.

Kobenan Kouassi Adjoumani aliteuliwa kushika nafasi nyingine ya waziri wa kilimo katika taifa hilo linaloongoza duniani katika uzalishaji wa cocoa.

Hali ya kisiasa kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi imeyumba kutokana na uamuzi wa Rais wa zamani Henri Konan Bedie kuvunja ushirikiano wa miaka 10 na utawala wa Ouattarawa Oktoba mwaka 2018.

Pia upo uwezekano wa kurudi tena nyumbani kwa kiongozi wa zamani Laurent Gbagbo baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya kimataifa - ICC ya The Hague.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG