Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 18:51

Rais wa FIFA aomba vita kati ya Russia na Ukraine visitishwe kwa mwezi mmoja


Rais wa FIFA Gianni Infantino

Rais wa shirikisho la kandanda duniani Gianni Infantino ametoa wito wa kusitishwa kwa mwezi mmoja vita vya Russia nchini Ukraine ikiwa ni sawa na wakati kombe la dunia linafanyika nchini Qatar.

Kiongozi huyo wa FIFA alisema hayo wakati wa chakula cha mchana kwenye mkutano wa viongozi wa mataifa 20 tajiri duniani G20 mjini Bali Indonesia leo jumanne.

Akiwahutubia viongozi hao, Infantino amesema kwamba mashindano ya kwanza ya kandanda duniani kufanyika mashariki ya kati yanaweza kuchochea kuchukuliwa hatua chanya, ili kuwasilisha ujumbe wa matumani.

Russia ndio ilianda michuano ya mwisho ya kombe la dunia 2018 na ikafika robo fainali , wakati Ukraine ni miongoni mwa nchi zinazojaribu kuanda fainali za mwaka 2030.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG