Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:45

Rais wa Cuba anaweza tembelea Marekani


Ikulu ya Marekani
Ikulu ya Marekani

Msemaji wa White House Josh Ernest, amewaambia wanahabari Alhamisi kwamba “siwezi kataa ziara ya Rais Castro.”

Marekani imesema inawezekana Rais wa Cuba Raul Castro akafanya ziara kutembelea White House, kukutana na Rais Barack Obama.

Msemaji wa White House Josh Ernest, amewaambia wanahabari Alhamisi kwamba “siwezi kataa ziara ya Rais Castro.”

Siku ya Jumatano viongozi hao walitangaza mipango ya nchi zao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baada ya kipindi cha nusu karne ya uhusiano mbaya ulionzia katika vita baridi.

Bwana Ernest, pia alisema inawezekana Rais Obama akafanya ziara Havana, Cuba, wakati nchi hizo mbili zinafungua ubalozi katika miji yao mikuu.

XS
SM
MD
LG