Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 17:09

Rais wa Benki ya Dunia atangaza kuondoka madarakani


Rais wa Benki ya dunia, David Malpass, Jumatatu amesema ataondoka kwenye nafasi yake ifikapo mwishoni mwa Juni.

Ametoa tangazo hili miezi kadhaa baada kutowajibika kwake kwa White House aliposhindwa kusema kama anakubaliana na mashauri ya kisayansi kuhusu kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani.

Malpass, aliyeteuliwa na rais msaafu wa Marekani, Donald Trump, ataondoka katika benki hiyo yenye malengo ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwa ni chini ya mwaka mmoja wa muhula wa miaka mitano.

Hakutoa sababu maalumu ya hatua yake hiyo bali alisema katika taarifa, baada ya kutafakari vyema ameamua kwenye kukabiliana na changamoto nyingine.

Katika taari waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, amemshukuru Malpass kwa huduma yake kwa kusema dunia ilinufaika na msaada wake madhubuti kwa Ukraine wakati wa uvamizi wa kinyume cha sheria wa Russia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG