Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:51

Rais wa Argentina atembelea Bahia Blanca kujionea hasara iliyosababishwa na kimbunga


Raiwa wa Argentina Javier Milei (Kulia) akiwa na makamau wa rais Victoria Villarruel.
Raiwa wa Argentina Javier Milei (Kulia) akiwa na makamau wa rais Victoria Villarruel.

Rais mpya wa Argentina Javier Milei pamoja na mawaziri kadhaa kutoka baraza lake Jumapili wamezuru mji wa bandari wa Bahia Blanca ili kujionea wenyewe hasara iliyosababishwa na kimbunga.

Takriban watu 13 waliuwawa mjini humo Jumamosi kufuatia mvua kubwa zilizoandamana na upepo mkali. Maafisa wamesema kwamba takriban watu 14 walijeruhiwa baada ya paa la kituo cha michezo kuporomoka wakati wa mvua hiyo.

Kimbunga hicho kiliendelea Jumapili hadi kwenye mji mkuu wa Buenos Aires ,wakati kikiangusha miti, kukata huduma za umeme, pamoja na kusababisha uharibifu mkubwa. Taarifa zimeongeza kwamba pia kimeuwa watu wawili kwenye taifa jirani la Uruguay.

Forum

XS
SM
MD
LG