Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 22:16

Rais Ruto anakutana na Rais Tshisekedi kuzungumzia usalama wa DRC


Baadhi ya wakaazi wa eneo la mashariki mwa DRC wakikimbia nyumba zao kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23
Baadhi ya wakaazi wa eneo la mashariki mwa DRC wakikimbia nyumba zao kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23

Rais Ruto atafanya mazungumzo na mwenzake Rais Felix Tshisekedi wa DRC kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya usalama mashariki mwa DRC ofisi yake imesema, kabla ya Ruto kuelekea Korea Kusini baadaye Jumatatu.

Rais wa Kenya William Ruto ataelekea mjini Kinshasa Jumapili ofisi yake imesema huku kukiwa na juhudi za kujaribu kuleta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ziara yake inakuja baada ya ziara ya mtangulizi wa Ruto, Uhuru Kenyatta, ambaye ni mpatanishi katika mzozo wa DRC kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ruto atafanya mazungumzo na mwenzake wa Congo, Felix Tshisekedi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya usalama mashariki mwa DRC, ofisi yake imesema, kabla ya kuelekea Korea Kusini baadaye Jumatatu.

Mapigano yamekuwa yakiendelea mashariki mwa nchi hiyo huku kundi la waasi la M23 likipiga hatua katika maeneo ya huko na kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao.

Kenya inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani katika siku zijazo, na pia imetuma wanajeshi nchini DRC kama sehemu ya kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha EAC.

Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta alisema Ijumaa kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye serikali yake inatuhumiwa na Kinshasa kwa kuliunga mkono kundi la M23 yuko tayari kusaidia katika juhudi za kuwashinikiza waasi kusitisha mapigano na kujiondoa katika ardhi waliyoiteka.

Wakati wa ziara yake huko mashariki wiki iliyopita, Kenyatta aliielezea hali huko kama "janga la kibinadamu".

XS
SM
MD
LG