Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 06:15

Rais Ramaphosa amsimamisha kazi mkuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitangaza bajeti ya ofisi ya rais katika bunge, mjini Cape Town, June 9, 2022. Picha ya AFP
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitangaza bajeti ya ofisi ya rais katika bunge, mjini Cape Town, June 9, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Alhamisi amemsimamisha kazi mkuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi wakati bunge linaandaa kikao kilichocheleweshwa kwa muda mrefu kusikiliza mashtaka yanayomkabili, ya kutaka kumng’oa mamlakani.

Busisiwe Mkhwebane aliteuliwa kuwa mlinzi wa mali ya umma na rais wa zamani Jacob Zuma.

Uteuzi wake ulionwa na wengi kama njama ya kumlinda Zuma dhidi ya tuhuma za ufisadi.

Kwa miaka minne, aliwasilisha malalamiko ya kuzuia mchakato wa kusikilizwa na bunge kwa makosa yanayomkabili, lakini hakufaulu.

Bunge lenye wabunge wengi kutoka chama cha Ramaphosa cha African National Congress ( ANC), mwezi uliopita lilikubaliana kuanzisha kikao cha kusikiliza mashtaka dhidi yake.

“Mkhwebane ataendelea kusimamishwa hadi mchakato katika bunge utakuwa umekamilika,” ofisi ya rais imesema katika taarifa.

Taarifa hiyo imejiri siku moja baada ya Mkhwebane kuanzisha uchunguzi juu ya madai kuwa Ramaphosa alificha wizi wa fedha ulitokea kwenye shamba lake mwaka wa 2020.

Mahasimu wa Ramaphosa wanasema kashfa hiyo imeonyesha kitendo cha utakatishaji wa fedha uliofanywa na rais huyo tajiri, wakidai kwamba majambazi waliiba pesa taslimu dola milioni 4 zilizokuwa zimefichwa ndani ya shamba lake.

Ofisi ya rais imesema naibu wa Mkhwebane ataendelea kushughulikia kesi zote ambazo hazijakamilika.

XS
SM
MD
LG