Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 14:03

Rais Ouattara atawazwa rasmi


Rais wa Ivory Coast President Alassane Ouattara akimpungia mkono rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy Mei 21, 2011 mjini Yamoussoukro

Sherehe za kumtawaza rasmi Alassane Outtara zafanyawa Yamoussoukro

Ivory Coast hatimaye imemtawaza rasmi rais Alassane Ouattara katika sherehe zilizocheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita kutokana na ghasia za kisiasa baada ya rais aliyemtangulia kukatalia madarakani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy walikuwa miongoni mwa viongozi wa nchi na wajumbe zaidi ya 20 waliohudhuria sherehe hizo Jumamosi katika mji mkuu Yamoussoukro.

Alipowasili mjhini humo, umamosi asubuhi, Bw. Sarkozy alisema alihisi ni jambo muhimu kwa demokrasia na kwa bara la Afrika kuwa nchini Ivory Coast kwa sherehe hizo.

Na ingawa Bw.Ouattara aliapishwa na kuingia rasmi ofisini mapema mwezi huu wa Mei, sherehe za Jumamosi ziliadhimisha enzi mpya kwa taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya mwongo wa msukosuko wa kisiasa na maasi yaliyoligawa taifa hilo mara mbili, na chaguzi zilizoahirishwa mara kwa mara.

Ghasia zilizuka tena mwezi Novemba mwaka jana baada ya uchaguzi wa urais, pale rais Laurent Gbagbo ambaye alikuwa madarakani tangu mwaka wa 2000 alipokataa kukubali kushindwa. Inakisiwa watu elfu tatu waliuawa katika mapigano yaliyotokana na mzozo wa uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG