Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 10:51

Rais Obama kuliwaza familia Newtown


Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn.
Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn.
Rais wa Marekani Barack Obama Jumapili atakwenda Newtown, jimbo la Connecticut kuliwaza wakazi wa mji uliokumbwa na msiba mkubwa baada ya mshambuliaji kuuwa watoto 20 wa shule ya Sandy Hook pamoja na watu wazima sita.

White House imesema rais Obama atakutana na familia za waliopoteza wapendwa wao na pia kuwashukuru wote waliokwenda shuleni humo kusaidia waathiriwa wa mkasa huo. Bw. Obama atazungumza Jumapili jioni kwenye mkusanyiko wa watu wanaomboleza pamoja na familia za waathiriwa.

Polisi wa Connecticut wamewatambulisha waliouawa wakiwemo wasichana 12 na wavulana wanane wote wa kati ya umri wa miaka 6 na 7.Watu wazima wote sita waliouawa walikuwa wanawake.

Afisa wa afya aliyekagua maiti zao alisema wote walipigwa risasi wakiwa hatua chache kutoka kwa muuaji huyo kabla hajajiuwa kwa risasi. Msiba huu wa kihistoria Marekani umegonga vichwa vya habari Marekani na nchi za Ulaya na bara Asia.
XS
SM
MD
LG