Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 13:13

Obama kutoa hotuba ya hali ya taifa Jumanne


Rais Barack Obama katika moja ya hotuba zake zilizopita za hali ya kitaifa.

Rais wa Marekani Barack Obama alisema kwamba “Marekani inaweza kufanya chochote kile alipokua anazungumzia mada ya hotuba yake ya mwisho juu ya hali ya kitaifa atakayoitoa Jumaane usiku.

Rais Obama na wapinzani wake wa chama cha Republican wanatofautiana katika tathmini ya miaka saba iliyopita na mapambano juu ya kile Marekani inachotaka kusonga mbele. Rais Obama anaona kumefanyika mafanikio na msingi thabiti unaofaa kujenga maendeleo.

Rais alisema biashara za Marekani hivi sasa zipo katika mwezi wa 70 mfululizo katika kubuni nafasi mpya za ajira kukiwa na zaidi ya ajira mpya milioni 14. Alisema wamefanya uwekezaji wa kihistoria katika nishati mbadala na kujiweka wenyewe katika njia ya baadae ya kupunguza hewa chafu ya carbon. Wa-Republican kwa muda mrefu wamekuwa wakikosoa rekodi ya kiuchumi ya bwana Obama kuwa inadumaza sana na itaendelea kudidimiza nchi.

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama

Wakati huo huo mkimbizi mmoja wa Syria aliyewasili hivi karibuni na mwanajeshi wa zamani wa Marekani, ambaye ni muislam watakuwa miongoni mwa wageni waalikwa wa White House, akikaa na mke wa rais, bi. Michelle Obama katika sehemu maalumu Jumanne usiku, wakati Rais Barack Obama akitoa hotuba yake ya mwisho juu ya hali ya taifa.

Wageni hao waliochaguliwa na mke wa rais ni Naveed Shah, muislam na mwanajeshi wa zamani wa Marekani ambaye alikuwa mtoto wakati wazazi wake walipohamia nchini marekani kutoka Pakistan. Pia atakuwepo Refaai Hamo kutoka Troy, Michigan watakaa pamoja na bi. Obama kusikiliza hotuba hiyo muhimu ya kihistoria.

Hamo aliwasili Detroit, Disemba 18 akiwa na watoto wake ambao watatu ni wasichana na mmoja mvulana baada ya kukaa miaka miwili nchini Uturuki.

XS
SM
MD
LG