Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 23:19

Rais Obama aondoka Marekani


picha ya Rais Obama

Atawasili kenya Ijumaa ambako atahudhuria mkutano wa dunia wa wajasiriamali mjini Nairobi.

Rais wa marekani Barack Obama ameondoka Alhamisi nchini kwake kwa ajili ya ziara nchini Ethiopia na Kenya mahali alipozaliwa baba yake, wakati pia akisisitiza kuhusu ukuaji wa uchumi wa Marekani na kuhusisha pia na nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la sahara.

Atawasili kenya Ijumaa ambako atahudhuria mkutano wa dunia wa wajasiriamali mjini Nairobi.

Baadae atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kutembelea Ethiopia . Makundi ya kutetea haki za binadamu yametoa mwito kwa rais Obama kutumia ziara yake kusisitiza marekebisho ya msingi ya haki za binadamu katika nchi zote.

Katika barua iliyoandikwa kwa Obama , kundi la jumuiya 14 zisizokuwa za kiserikali na wataalamu binafsi wamesema Serikali za kenya na Ethiopia zinakabiliwa na tishio kubwa la usalama lakini kuna wasiwasi jinsi nchi hizo zinavyojibu kwa kutumia hatua za usalama za unyanyasaji na kuongeza juhudi kuzuiya jumuiya za kiraia na vyombo vya habari binafsi.

XS
SM
MD
LG