Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:21

Rais Obama ampongeza Alassane Ouattara


Rais mteule wa Ivory Coast Alassane Ouattara
Rais mteule wa Ivory Coast Alassane Ouattara

Taarifa ya White House inaeleza kwamba viongozi hao wawili walijadili juu ya umuhimu wa kuanzisha tena biashara kusaidia Ivory Coast

Rais wa Marekani Barack Obama amezungumza kwa simu na rais mpya wa Ivory Coast Alassane Ouattara na kumpongeza kwa kuchukua madaraka.

White house imesema Bw. Obama alimpigia simu Ouattara Jumanne siku moja baada ya wapiganaji wake kumkamata kiongozi wa zamani Laurent Bagbo ambaye alikataa kuacha madaraka.

Taarifa ya White House inaeleza kwamba viongozi hao wawili walijadili juu ya umuhimu wa kuanzisha tena biashara ili kusaidia kufufua tena uchumi Ivory Coast. Inaeleza walizungumzia pia juu ya haja kuhakikisha watu walofanya mashambulio mnamo miezi ya ghasia za kisiasa wanawajibika, bila ya kujali ni wa upande gani.

Siku ya Jumanne pia, Ufaransa ilisema itaipatia Ivory Coast kiasi cha dola million 580 kusaidia raia wake kuanza upya huduma za umma na kufufua uchumi wake.

Waziri wa fedha Christine Lagarde alisema fedha zitagharimia matumizi ya dharura ya raia, mji wa Abidjan na huduma muhimu za umma.

Katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa Ban Ki-moon kwa upande wake alitoa wito kwa Ivory Coast kuchukua nafasi hii ya kihistoria kwa ajili ya upatanishi wa kitaifa kufuatia kukamatwa kwa Bw Gbagbo. Bw. Ban alizungumza na Outtara Jumatatu na kusisitiza haja ya kuhakikisha hakuna ulipizaji kisasi dhidi ya wafuasi wa Gbagbo.

Umoja wa Mataifa utaendelea kuwalinda raia na kusaidia serikali kudumisha tena utawala wa sheria.

XS
SM
MD
LG