Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 06:13

Rais wa Nigeria amfuta kazi mshauri wake wa masuala ya ugaidi


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, katikati, akizungumza na waandishi wa habari hapo Agosti 27, 2001 kwenye ofisi za Umoja Mataifa mjini Abuja ambazo zilishambuliwa na bomu.

Serikali ya Nigeria yaahidi kupambana na kuudhibiti ugaidi.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amemfukuza kazi mshauri wake wa masuala ya kupamba na ugaidi wiki mbili baadaya mlipuko wa bomu kuua takriban watu 23 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu, Abuja.

Msemaji wa rais, Rueben Abati hakutoa maelezo zaidi kwanini Zakari Ibrahim ameondolewa kwenye wadhifa wake.

Msemaji huyo amesema Meja Jenerali Sarkin Bello ametajwa kuchukua nafasi ya Ibrahim.

Nigeria imekumbwa na ongezeko la wimbi la mashambulizi ya kutisha katika miezi ya karibuni, ikiwemo shambulizi la bomu la kujitoa mhanga la kwenye gari hapo Agosti 26 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini abuja. Mbali ya wale waliouawa, zaidi ya watu 80 walijeruhiwa na shambulizi hilo.

Kundi la kiislamu lenye msimamo mkali la Boko Haram, limedai kuhusika na shambulizi hilo. Maafisa walilaumu Boko Haram kwa dazeni ya mabomu na mashambulizi mengine nchinihumo, hasa katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno.

Serikali ya Nigeria imekuwa kwenye shinikizo kali la kumaliza kabisa mlolongo wa mabomu na mauaji ambayo yanadaiwa kufanywa na Boko Haram.

Kundi hilo lenye msimamo mkali linataka sheria za kiislamu zitumike kote katika taifa hilo la Afrika lenye watu wengi.

Rais Jonathan ameapa kuudhibiti ugaidi nchini Nigeria.

XS
SM
MD
LG