Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:13

Rais mteule wa Gambia kuapishwa Januari 19


Rais mteule wa Gambia Adama Barrow
Rais mteule wa Gambia Adama Barrow

Msemaji wa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow alithibitisha Jumapili kwamba Barrow ataapishwa Januari 19 licha ya rais Yahya Jammeh kukataa kuondoka madarakani. “Utawala wa jammeh utakwisha januari 19 na tarehe hiyo hiyo utawala wa rais mteule Barrow utaanzia hapo.

Hakuna kitakachobalika, ataapishwa na kuanza kazi tarehe hiyo bila kushindwa”, alisema hayo msemaji Mai Fatty kupitia shirika la habari la kimataifa la AFP.

Barrow alikwenda Senegal baada ya wanachama wa ECOWAS kushindwa kumshawishi Jammeh kukabidhi madaraka wakati kipindi chake cha utawala wa miaka mitano kitakapokwisha wiki chache kuanzia sasa.

Barrow yuko Dakar kuanzia leo Jumapili. Haijaelezwa bayana ni kwa nini rais mteule Barrow amekwenda Senegal lakini vyanzo vya habari vinasema ni kutokana na hofu ya kukosa usalama. Rais wa Senegal alikubali ombi la kumpokea Barrow kutoka kwa rais wa Liberia Ellen Jonhson Sirleaf mwenyekiti wa ECOWAS mpaka kipindi cha kuapishwa kitakapofika.

Barrow alikutana Jumamosi nchini Mali na viongozi wa nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kila mwaka kati Ufaransa na Afrika kwenye mji mkuu wa Bamako. Marais wa Ufaransa na Mali Ibrahim Boubacar Keita na Francois Hollande wote walitoa wito kwa Jammeh kujiuzulu wakati kipindi chake cha miaka mitano kitakapokamilika.

XS
SM
MD
LG