Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 16:17

Rais mpya wa Sri Lanka aapishwa, awaomba Tamil na Waislam kumpa ushirikiano


Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa katika hafla ya kuapishwa kwake huko Anuradhapura, Sri Lanka Novemba 18, 2019. REUTERS/Dinuka Liyanawatte

Rais mpya wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaska ameapishwa kuwa rais Jumatatu.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa hafla ya kuapishwa kwake imefanyika kwenye hekalu la Kibudha la Runawell lililoko mji wa kaskazini.

Rajapaska ameziomba jamii za walio wachache kutoka Tamil na Waislam ambao hawakumpigia kura kushirikiana naye katika kujenga taifa.

Jamii zote mbili wakati wa kampeni zilieleza wasiwasi wao kutokana na ushindi wake kwa sababu ya msimamo wake mkali wa kijeshi wakati akiwa chini ya serikali ya kaka yake mkubwa, rais wa zamani Mahinda Rajapaska.

Wakati wa kuapishwa kwake, rais huyo mpya ameahidi kuwa suala la usalama wa ndani litakuwa kipaumbele kwenye utawala wake.

Sri Lanka ilikumbwa na mashambulizi ya kujitoa muhanga wakati wa sikukuu ya Pasaka ambapo watu 269 waliuawa.

Kiongozi huyo mpya mwenye umri wa miaka 70 aliongoza operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Tamil miaka 10 iliyopita. Rajapaska alimshinda mpinzani wake Sajith.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG