Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 09:55

Rais mpya wa Namibia anasema hana mpango wa kuwania urais


Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba akila kiapo kufuatia kifo cha Rais Geingob.
Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba akila kiapo kufuatia kifo cha Rais Geingob.

Matamshi ya Mbumba yanamaanisha Makamu wa Rais mpya Netumbo Nandi-Ndaitwah anaweza kuwania nafasi ya urais

Nangolo Mbumba ni rais wa muda wa Namibia nchi iliyopo kusini mwa Afrika. Aliapishwa Jumapili kufuatia kifo cha Rais Hage Geingob kilichotokea mapema siku hiyo katika hospitali moja mjini Winhoek. Geingob alitangaza mwezi Januari kwamba alikuwa na saratani.

Mbumba alisema Jumapili kwamba hana mpango wa kuwania urais katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu. Hiyo inamaanisha kuwa makamu wa rais mpya Netumbo Nandi-Ndaitwah anaweza kuwania nafasi ya urais. Kama atashinda, atakuwa rais wa kwanza mwanamke katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Hata hivyo anaweza kukabiliana na wapinzani ndani ya SWAPO, chama chake cha siasa. The South West Africa People’s Organisation au SWAPO kimekuwa madarakani nchini Namibia tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1990. Rais Geingob hivi karibuni ali-ikosoa Ujerumani kwa kuiunga mkono Israel dhidi ya mashtaka ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Geingob alisema Ujerumani ilifanya mauaji ya kimbari nchini Namibia katika miaka ya 1800, na kuua maelfu ya Waafrika.

Forum

XS
SM
MD
LG