Rais mpya wa Guatemala Bernardo Arevalo ameahidi mapema Jumatatu kupambana na rushwa na kusimama imara dhidi ya utawala wa kiimla duniani, katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa.
Hatutaruhusu taasisi zetu kukumbwa na rushwa na kutokhofia kushtakiwa,” alisema katika sherehe ya kuapishwa iliyofanyika Guatemala City, kwa zaidi ya saa tisa baada ya juhudi za mwisho za kuzuia rushwa na kuingia madarakani.
Mbunge huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 65, mwanadiplomasia na mwanasosholojia aliondoa hasira kubwa wakati alipojitosa na kushinda uchaguzi mwezi Agosti mwaka jana, na kuwafariji wapiga kura waliochoshwa na rushwa katika moja ya mataifa masikini zaidi ya Amerika Kusini.
Alikula kiapo baada ya kuzuia jaribio la kumzuia kuchukua madaraka ikiwa ni pamoja na waendesha mashtaka wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa ambao wanahusiana kwa karibu na tabaka la kisiasa na kiuchumi la nchi hiyo.
Forum