Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 02:04

Rais Macron wa Ufaransa ameelezea sheria inayoongeza umri wa kustaafu


Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron

Rais Macron alisema katika mahojiano ya nadra ya televisheni. Lakini hakuna njia nyingine za kusawazisha suala hili. Mageuzi haya ni muhimu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo Jumatano alisema sheria mpya isiyopendwa ambayo inaongeza umri wa kustaafu ni muhimu na itaanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu. Unadhani ninafurahia kufanya mageuzi haya? Hapana," Macron alisema katika mahojiano ya nadra ya televisheni. Lakini hakuna njia nyingine za kusawazisha suala hili.

Mageuzi haya ni muhimu. Hadi serikali iliposukuma mswaada wa pensheni bila kupigiwa kura, maandamano ya kuupinga mswaada utakaosukuma umri wa kustaafu kwa miaka miwili zaidi hadi umri wa miaka 64 yalikuwa yamekusanya umati mkubwa wa watu katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na vyama vya wafanyakazi Ufaransa.

Lakini tangu uamuzi wa serikali kuepuka kura bungeni wiki iliyopita, maandamano mjini Paris na kwingineko yameshuhudia mapipa ya takataka na vizuizi vikichomwa moto kila usiku huku kukiwa na misukosuko na polisi.

XS
SM
MD
LG