Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:09

Rais Kiir na Machar wakubaliana kuanza mazungumzo


Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wanawatuma wawakilishi wao Ethiopia kwa mazungumzo ya amani, huku ghasia zikiendelea katika mji wa Bor nchini mwao.

Serikali ya Ethiopia imesema rais Kiir na aliyekuwa zamani makamu rais wake Machar wamekubali kutuma wawakilishi wao leo Jumanne mjini Addis Ababa.Lakini licha ya makubaliano hayo mapigano bado yanaendelea katika mji wa Bor, mji mkuu wa jimbo la Jong’lei. Machar na wafuasi wake wanasema wapiganaji watiifu kwake wameuteka tena mji huo.

Waasi hao waliudhibiti kwa muda mfupi mji huo mapema mwezi huu. Hakuna tamko la mara moja kutoka upande wa serikali ikiwa kweli waasi wameudhibiti ten mji wa Bor.

Ghasia za kikabila zilizuka mapema mwezi huu baada ya rais Kiir ambaye ni wa kabila la Dinka kumshtumu Machar ambayo ni wa kabila la Nuer kwa kupanga jaribio la kupindua serikali yake.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na maelfu kulazimishwa kuhama makazi yao.

Wiki jana viongozi wa ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na shirika la IGAD waliweka masharti ya hadi leo Jumanne kwa pande zote mbili kufanya mazungumzo ya ana kwa ana, kwa lengo la kumaliza mgogoro baina yao. Machar amesema ujumbe wake utamjumwisha Rebecca Nyadeng Garang, mjane wa John Garang na mwanzilishi wa kudni la Sudan Peopl’es Liberation Movement–(SPLM)
XS
SM
MD
LG