Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 14:18

Rais Jakaya Kikwete ashinda awamu ya pili


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete atangazwa mshindi.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete atangazwa mshindi.

Rais Jakaya Kikwete ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais nchini Tanzania huku mpinzani Dr. Slaa apinga matokeo hayo.

Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imetangaza matokeo ya uchaguzi wa rais ambapo Rais Jakaya Kikwete amepata ushindi wa asilimia 61.17 na kurudi tena madarakani kwa muhula wa pili nchini humo.

Kwa mujibu wa tume hiyo iliyotangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Karimjee Dar es salaam mbele ya wagombea wote isipokuwa Dr.Wilbroad Slaa ambaye amesema anapinga matokeo hayo.

Matokeo hayo ni kama ifuatavyo :

Kikwete Jakaya Mrisho wa CCM kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17 .

Dr.Slaa Wilbroad Peter wa CHADEMA kura 2271942 sawa na asilimia 26.34

Lipumba Ibrahim Haruna 695,667 sawa asilimia 8.

Rungwe Hashim Spunda NCCR-MAGEUZI 26,338 sawa na asilimia 0.31.

Kuga Peter Mziray asilimia APPT Maendeleo asilimia 1.12

Mughaiywa Mutamwega Bhatt TLP 17,428 asilimia 0.20

Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa UPDP 13,176 asilimia 0.15

XS
SM
MD
LG