Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ana muhula mpya wa miaka mitano baada ya kushinda uchaguzi wa marudio ambao wanachama wa upinzani walitumai huenda utamuondoa madarakani kufuatia ghasia zinazohusu ongezeko la gharama ya maisha.
Erdogan alishinda Jumapili katika mzunguko wa pili wa upigaji kura kwa asimilia 52 akifuatiwa na mpinzani mkuu Kemal Kilicdaroglu aliyepata asilimia 47.8 ya kura. "Ninamshukuru kila mwanachama katika taifa letu kwa kuendelea kuniamini kuchukua majukumu ya kui ongoza nachi hii kwa mara nyingine katika kipindi cha muhula wa miaka mitano", Erdogan aliwaambia wafuasi wake.
"Napenda kuwashukuru raia wetu wote ambao walionyesha nia zao za dhati kwa mustakbali wa baadae ya taifa hili, kwa ajili yao na watoto wao, kwa kupiga kura kwenye uchaguzi huu".
Kilicdaroglu hakupinga matokeo lakini aliuita uchaguzi usio sahihi katika miaka ya karibuni.
Forum