Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 12, 2025 Local time: 08:31

Rais Erdogan ameshinda uchaguzi wa Uturuki


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameshinda duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika Jumapili.

Alizungumza na wafuasi wake baada ya matokeo ya awali yasiyo rasmi kumpa asilimia 52 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 48 alizopata mpinzani wake Kemal Kilicdaroglu.

“Namshukuru kila mwanachama wa taifa letu kwa kunikabidhi jukumu la kuongoza nchi hii kwa mara nyingine tena kwa miaka mitano ijayo,” alisema Erdogan, ambaye alikuwa akiwania muongo wa tatu madarakani.

Alionekana kama mshindi wa mbele kuelekea upigaji kura wa Jumapili baada ya kushindwa kwa idadi ndogo katika raundi ya kwanza ya uchaguzi.

Erdogan na Kilicdaroglu walisema katika mikutano ya dakika za mwisho Jumamosi kwamba kujitokeza kwa wapiga kura hasa wafuasi wao kutakuwa muhimu kwa matokeo ya kura ya urais

Forum

XS
SM
MD
LG