Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 14:03

Rais Bio wa Siera Leone ametangaza hali ya dharura ya taifa


Rais wa Siera Leone, Julius Maada Bio

Inaripotiwa kwamba zaidi ya kesi 8,000 za awamu ya tatu zinazohusiana na manyanyaso ya kijinsia zilizoripotiwa nchini Siera Leone mwaka 2018 ziliwahusisha watoto.

Rais wa Siera Leone, Julius Maada Bio ametangaza hali ya dharura ya taifa kwa sababu ya kuongezeka idadi kubwa ya ghasia za ubakaji na ngono nchini humo.

Rais Bio alisema mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya mashtaka ya manyanyaso ya ngono dhidi ya watoto atakabiliwa na kifungo cha maisha jela. Zaidi ya kesi 8,000 za awamu ya tatu zinazohusiana na manyanyaso ya kijinsia zilizoripotiwa nchini Siera Leone mwaka 2018 ziliwahusisha watoto.

Idadi kamili ya kesi inadhaniwa kuwa juu lakini mazungumzo kuhusu uhalifu wa ngono kwa jumla yamekuwa mwiko katika taifa hilo lililopo Afrika magharibi. Rais Bio wakati akitangaza hali ya dharura ya kitaifa alisema “Sisi kama taifa, lazima tusimame na kuelezea janga hili”.

Alieleza kwamba hospitali za serikali zitatoa huduma ya bure ya matibabu kwa waathirika wa ubakaji na unyanyasaji wa ngono. Katika kuongezea Bio alisema kitengo maalumu cha polisi kwa waathirika wa ubakaji na ghasia za ngono pamoja na mahakama maalumu zitaanzishwa kuharakisha kushughulikia kesi hizi.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG