Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:18

Rais Biden wa Marekani amefanya ziara Ukraine na kuahidi msaada zaidi wa kijeshi


Rais wa Marekani Joe Biden (L) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Marekani Joe Biden (L) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Akizungumza akiwa pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika makazi ya rais mjini Kyiv, Biden alitangaza msaada mpya wa Marekani wa dola milioni 500 zikiwemo risasi za kivita na za kupambana na vifaru. Pia alisema kutakuwa na vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia wiki hii

Rais wa Marekani Joe Biden leo alifanya ziara Jumatatu ambayo haijatangazwa nchini Ukraine siku chache kabla ya nchi hiyo kuadhimisha mwaka mmoja wa uvamizi wa Russia, Biden alisema alikuwa huko kuonyesha uungaji mkono wetu kwa uhuru wa taifa hilo, mamlaka yake na uadilifu wa eneo.

Akizungumza akiwa pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika makazi ya rais mjini Kyiv, Biden alitangaza msaada mpya wa Marekani wa dola milioni 500 zikiwemo risasi za kivita na za kupambana na vifaru. Pia alisema kutakuwa na vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia wiki hii.

Mwaka mmoja baadae, Kyiv inasimama. Ukraine inasimama. Demokrasia inasimama alisema Biden. Wamarekani wanasimama na nyinyi na ulimwengu unasimama na wewe. Biden alizungumza kuhusu kuuleta pamoja muungano wa zaidi ya nchi 50 kulisaidia jeshi la Ukraine na kuunganisha uchumi unaoongoza kuweka gharama ambazo hazijawahi kutokea kwa uchumi wa Russia.

XS
SM
MD
LG