Rais wa Marekani Joe Biden anaelekea Florida Jumamosi kuangalia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Idalia na kuwafariji watu walioathiriwa na dhoruba hiyo, lakini hatakutana na Gavana wa jimbo hilo Ron DeSantis Mrepublican na mpinzani mtarajiwa kwenye kinyang’anyiro cha urais.
Biden mdemokrat aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa kuwa angekutana na gavana huyo wakati wa safari yake lakini msemaji wa DeSantis Jeremy Redfern alisema baadaye kwamba hakuna mkutano uliopangwa na maandalizi ya usalama pekee kwa ajili ya mkutano huo huenda yatazuia shughuli za kurejesha hali ya kawaida katika jimbo hilo.
DeSantis mwenye umri wa miaka 44, anawania uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha Republican kwa mwaka 2024 ili kumuondoa madarakani rais Biden kutoka White House, lakini yuko nyuma ya Rais wa zamani Donald Trump katika kura za maoni. Biden mwenye umri wa miaka 80 anagombea tena kwa muhula wa pili.
Forum