Rais wa Marekani Joe Biden anaadhimisha siku ya mashujaa leo Mei 29 kwenye makaburi ya kitaifa ya Arlington mahala ambako kiasi cha watu 400,000 wapiganaji na wategemezi wao wanaostahiki wamezikwa huko.
Ataweka shada la maua kwenye Kaburi la Askari Asiyejulikana na kulihutubia taifa. Leo Jumatatu ni maadhimisha ya miaka 155 ya siku ya mashujaa nchini marekani wakati taifa linatoa heshima kwa watu ambao wamepoteza maisha yao katika kulihudumia taifa.
Siku hii inatambuliwa kila mwaka katika Jumatatu ya mwisho ya mwezi Mei.
Sherehe hii ilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1868 wakati nchi ilijiponya kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya marekani. Imekuwa sikukuu ya serikali kuu kwa Zaidi ya karne moja baadae katika mwaka 1971.
Forum