Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 13:17

Rais Biden ameahirisha ziara ya Colorado ili kushughulikia usalama wa ndani wa taifa


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Maafisa wa Marekani na Israel wanajadili uwezekano wa ziara ya haraka ya Biden kwenda Israel, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, chanzo kinachofahamu suala hilo kimesema Jumapili

Rais wa Marekani Joe Biden ameahirisha ziara yake katika kiwanda cha upepo kwenye jimbo la Colorado, Marekani siku ya Jumatatu na kuendelea kuwepo White House kwa ajili ya mikutano ya usalama wa taifa, White House imesema huku Biden akifikiria kufanya ziara nchini Israel kati-kati ya mzozo na Hamas.

Maafisa wa Marekani na Israel wanajadili uwezekano wa ziara ya haraka ya Biden kwenda Israel, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, chanzo kinachofahamu suala hilo kimesema Jumapili.

Ziara ya Biden kuonyesha uungaji mkono kwa mshirika mkubwa wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati itafuatia ziara kama hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ambaye kwa sasa yuko katika eneo hilo.

Juhudi za kidiplomasia zimekuwa zikiendelea kupata msaada wa kuingia katika eneo hilo, ambalo limevumilia mashambulizi ya mabomu ya Israel tangu shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel na wanamgambo wa Hamas ambalo liliuwa watu 1,300 ikiwa ni siku moja ya umwagaji damu mkubwa katika historia ya taifa hilo ya miaka 75.

Forum

XS
SM
MD
LG