Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:39

Rais Biden aanza ziara ya Asia akiangazia uhaba wa chip za kompyuta


Rais Joe Biden akipokelewa na mfanyakazi wa kampuni ya Samsung Electronics Pyeongtaek akiwa na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, Friday, May 20, 2022, mjini Pyeongtaek, Korea Kusini. (AP Photo/Evan Vucci)
Rais Joe Biden akipokelewa na mfanyakazi wa kampuni ya Samsung Electronics Pyeongtaek akiwa na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, Friday, May 20, 2022, mjini Pyeongtaek, Korea Kusini. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais ametembelea kiwanda cha Samsung ambacho kitakuwa mfano wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vingine vya kielectronic kutoka kampuni nyingine inayopanga kufunguliwa Texas hapa Marekani.

Ziara hiyo ilikuwa kipaumbele cha ndani cha Biden katika juhudi za kuongeza usambazaji wa chip za kompyuita.

Uhaba wa vifaa hivyo maarufu kama semiconductor mwaka 2021 uliathiri sekta ya magari , vifaa vya jikoni, na bidhaa nyingine na kusababisha mfumuko wa bei kote duniani na kudhoofisha uungwaji mkono wa umma kwa Biden kutoka kwa wapiga kura.

Biden atakabiliana na masuala mengi ya sera za mambo ya nje wakati wa ziara yake ya siku tano nchini Korea Kusini na Japan, lakini pia aliandaa ratiba iliyokusudiwa kwa uwazi kushughulikia maswala ya watazamaji wake nyumbani pia.

Rais mpya wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol alisalimiana na Biden katika kiwanda hicho Korea Kusini.

Yoon ni mwanasiasa mpya amekuwa rais wa taifa hilo baada ya kuchaguliwa mara ya kwanza kuingia madarakani kiasi cha zaidi ya wiki moja tu iliyopita.

XS
SM
MD
LG