Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:49

Raila Odinga afanyiwa upasuaji


Waziri Mkuu Raila Odinga, kulia, akiwa na rais Mwai Kibaki
Waziri Mkuu Raila Odinga, kulia, akiwa na rais Mwai Kibaki

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amefanyiwa operesheni ndogo ya kichwa baada ya kulazwa hospitali Jumatatu.

Madaktari Kenya wanasema Waziri Mkuu Raila Odinga amefanyiwa operesheni ndogo ya kichwa Jumanne kuondoa shinikizo katika ubongo.

Daktari wa upasuaji Oluoch Olunya aliwaambia waandishi Bwana Odinga anaendelea vizuri baada ya operesheni hiyo katika hospitali ya Nairobi. Waziri Mkuu huyo alilazwa hospitali hapo Jumatatu baada la kulalamika uchovu wa kupita kiasi.

Hospitali hiyo inasema Bwana Odinga pia alikuwa akilalamika kuumwa sana na kichwa, na anakumbuka kuwa aliwahi kujigonga kichwa katika mlango wa gari wiki kadha zilizopita.

Madaktari wanasema waliona uvimbe nje ya ubongo wake na "katika muda mfupi wakakubaliana kuwa ni lazima kufanya operesheni ndogo upande wa kushoto wa kichwa" cha kiongozi huyo. Bwana Odinga ana umri wa miaka 65.

XS
SM
MD
LG