Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:30

Nina hakika tume ya uchaguzi itang'atuka, Raila aambia VOA

Kiongozi wa Muungano wa upinzani wa Kisiasa nchini Kenya, Raila Odinga, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba licha ya serikali kutumia nguvu na  gesi ya kutoa machozi kwa wafuasi wake amabo wamekuwa wakiandamana, ana imani kwamba Mwenyejkiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Izaak Hassan na majkamishna wote wa tume hiyo, watang'atuka kabla ya uchaguzi wa 2017.

Kiongozi wa Muungano wa upinzani wa Kisiasa nchini Kenya, Raila Odinga, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba licha ya serikali kutumia nguvu na gesi ya kutoa machozi kwa wafuasi wake amabao wamekuwa wakiandamana, ana imani kwamba Mwenyejkiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, Bw Izaak Hassan, na majkamishna wote wa tume hiyo, watang'atuka kabla ya uchaguzi wa 2017.

Wafuasi wa muungano huo wa CORD, kwa mara ya pili kwa muda wa wiki mbili, walifanya maandamano nje ya jengo la Anniversary Towers, ambalo ni makao makuu ya tume hiyo.

Bw Odinga, aliyezungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kutoka Nairobi, Kenya, alisema Wakenya wengi wamekosa imani na tume hiyo ya IEBC na ni lazima iondoke au iondolewe afisini. Alisema polisi waliwatupia waandamanaji gesi ya kutoa machozi waandamanaji hao licha ya kufanya maandamano kwa njia ya utulivu.

"Nadhani hawakufurahia walipoona tunafanya maandamano kwa utulivu,' alisema Odinga.

Sikiliza mahojiano hapa kati ya Bwana Odinga na BMJ Muriithi:

please wait

No media source currently available

0:00 0:11:08 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG