Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 04:50

Raila awataka wafuasi wake kususia kazi Jumatatu


Maafisa wa polisi walinda doria mjini Nairobi baada ya ghasia kuzuka kufuatia uchaguzi wa mwaka wa 2017.

Kiongozi  wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, Jumapili aliwataka wafuasi wake kususia kazi siku ya Jumatatu kama moja ya njia za kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyikia siku ya Jumanne.

Aidha Odinga alisema kwamba atatangaza hatua ambayo muungano wa National Super Alliance (NASA) utachukua mnamo siku ya Jumanne kufuatia uchaguzi huo ambao muungano huo unadai kwamba uligubikwa na dosari na kwamba haukuwa wa haki na kweli.

Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, mjini Nairobi, kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, Odinga alidai kuwa serikali ilikuwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani hata kabla ya kutangazwa matokeo.

Watu kadha wameripotiwa kuuliwa katika maeneo tofauti ya mji wa Nairobi na Kisumu kufuatia makabiliano na maafisa wa kulinda usalama baada ya wafuasi wa upinzani kujitokeza kulalamikia matokeo ya uchaguzi, huku baadhi yao wakiripotiwa kuzua ghasia na kupora mali.

Rais Uhuru Kenyatta, aliyekuwa anagombea muhula wa pili kwa tikiti ya chama cha Jubilee alitangazwa mshindi Ijumaa usiku baada ya siku tatu za kujumuisha kura katika zoezi ambali lilitajwa na waangalizi huru wa kimataifa kama lililokuwa wazi na huru.

Kulingana na IEBC, Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku mpinzani wake wa karibu, Raia Odinga akizoa kura 6,762,224.​ Wagombea wengine sita walipata jumla ya kiasi kidogo mno cah kura zilizopigwa.

Tangu kura zilipoanza kuhesabiwa Jumanne jioni, muunganbo wa Nasa ulikuwa unashikilia kwamba zoezi hilo lilikuwa limekumbwa na dosari, pamoja na kulalamika kwamba mfumo wa kidijitali wa tume hiyo ulikuwa umedukuliwa.

Wakati huo huo, aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ametoa wito kwa Bw Odinga kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.

Annan alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya kufuatia uchaguzi uliozua vurugu na kupelekea kuuawa kwa zaidi ya watu 1,000 manomo mwaka wa 2007.

"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," Annan alisema kupitia taarifa siku ya Jumapili.

"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi hapo mbeleni," aliongeza mwanadiplomasia huyo.

Hatua ya Odinga kutoenda mahakamani kuwasilisha malalamisi yake imekosolewa na baadhi ya wachambuzi wa kisiasa, baadhi yao wakiema kuwa mwansaiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 ana nia ya kuitumbukiza Kenya kwenye hali ya taharuki na ghasia.

Tangu kutangazwa mshindi na tume ya IEBC, rais Kenyatta hajazungumzia ghasia zinazoendelea moja kwa moja. Hata hivyo, alisema kwenye hotuba yake katika bustani za Bomas of Kenya kwamba angewataka wapinzani wake kujiunga naye na kujenga taifa.

"Namuuliza ndugu yangu mkubwa, Raila Amolo Odinga, kujiunga nami kwani nchi hii ni yetu sote," alisema Kenyatta.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG