Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 19:54

Raia wa Romania aliyetekwa nyara Burkina Faso tangu 2015 aachiliwa huru


Mlinzi wa Burkina Faso akishika doria kwenye mgodi wa Tambao ambapo raia wa Romania alitekwa nyara 2015.

Wizara ya mambo ya nje ya Romania imesema Jumatano kwamba raia wa taifa hilo aliyetekwa nyara kaskazini mashariki mwa  Burkina Faso  mwaka 2015 wakati akifanya kazi kwenye migodi ameachiliwa huru.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Lulian Ghregut aliyekuwa na umri wa miaka 39 wakati alipotekwa na kundi la wanamgambo lenye uhusiano na al Qaida, allikuwa akifanya kazi kama mlinzi kwenye mgodi, ameachiliwa akiwa salama na sasa yupo nchini Romania.

Taarifa kwa vyombo vya habari imewashukuru wote walioshiriki katika kuachiliwa kwake haswa serikali ya Morocco, kwa msaada muhimu waliotoa katika suluhisha kesi hiyo, iliyokuwa ya mkanganyiko, ingawa hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Ghergut alikuwa mateka wa kwanza kurekodiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Kutekwa nyara kwake 2015 kulifanyika wakati ambapo makundi yenye silaha yenye misimamo mikali yalikuwa na harakati nyingi kote katika eneo la Sahel barani Afrika chini ya jangwa la Sahara.

Forum

XS
SM
MD
LG