Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:29

Tehran: Raia wa New Zealand waandishi wa blogi waruhusiwa kuondoka Iran


Bridget Thackwray na mkewe Topher Richwhite
Bridget Thackwray na mkewe Topher Richwhite

Maafisa wa New Zealand wamesisitiza hakun makubaliano yaliyofikiwa  juu ya kuruhusiwa raia wake wawili kuondoka nchini  Iran. Maelezo machache yanatolewa kuhusu kesi ya familia hiyo ya New Zealand, ambao walikuwa wanaeleza kuhusu safari yao nchini Iran kwenye  mitandao ya kijamii.

Mapema mwaka huu, raia wa New Zealand Topher Richwhite, mtoto wa mmoja wa matajiri wakubwa nchini New Zealand, na mkewe Bridget Thackwray, waliitembelea Iran wakikaidi ushauri rasmi kutoka serikali huko Wellington.

Serikali iliwasihi raia wake kutokwenda Iran, ambapo kifo cha Mahsa Amini kilichochea maandamano na ghasia za kiraia.

Msichana huyo wa miaka 22 alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kupuuza kanuni kali za kufunika kichwa.

Maafisa wa New Zealand wamesema safari ya Richwhite na Thackwray nchini Iran ilikuwa imesitishwa na mamlaka za Iran na wameruhusiwa tu kuondoka nchini kwa msaada wa serikali ya Wellington.

Maafisa wa serikali wanasisitiza hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika kuwaruhusu wawili hao kuondoka.

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand Nanaia Mahuta aliiambia radio ya New Zealand katika kipindi cha Checkpoint kuwa mazungumzo na Iran yalikuwa magumu na yenye hisia kali.

XS
SM
MD
LG