Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 00:52
VOA Direct Packages

Raia wa Marekani aliyejiunga na ISIS nchini Syria apewa kifungo cha miaka 20 jela


Washukiwa wa Islamic State wakiwa wameshikiliwa Libya. Picha ya maktaba
Washukiwa wa Islamic State wakiwa wameshikiliwa Libya. Picha ya maktaba

Raia mmoja wa Marekani aliyehamia Syria pamoja na familia yake ili kujiunga la kundi la kigaidi la Islamic State amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.

Emraan Ali mwenye umri wa miaka 55 raia wa Marekani aliyezaliwa Trinidad na Tobago alihukumiwa Jumanne wiki iliyopita kwenye mahama ya serikali mjini Miami, Florida kulingana na rekodi za mahakama.

Novemba mwaka jana Ali alikubali makosa ya kutoa msaada kwa kundi la kigaidi la kigeni. Kulingana na rekodi hizo, Ali alisafirisha familia yake kutoka Trinidad and Tobago hadi Brazil na kisha kuelekea Uturuki kabla ya kuingia Syria Machi 2015.

Anasemekana kueleza watoto wake kwamba walikuwa likizoni, ingawa nia yake ilikuwa kijiunga na Islamic State, kulingana na muongoza mashitaka. Ripoti zimeongeza kwamba yeye na familia yake walisajiliwa kwenye IS mara baada ya kuingia Syria, wakati pia akipewa mafunzo ya kidini na kijeshi akiwa Pamoja na wanachama wengine wanaotumia lugha ya Kiingereza.

XS
SM
MD
LG