Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 15:26

Raia wa Malaysia wanapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali


Wapiga kura katika kituo cha Malacca nchini Malaysia

Kambi ya mageuzi ya kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim inatabiriwa kuongoza lakini huku kambi tatu kuu zikiwania kura wachambuzi wanasema ni vigumu kutabiri matokeo na yanaweza kushuhudia miungano mipya ikiundwa ikiwa hakutakuwa na mshindi wa moja kwa moja

Zoezi la kuhesabu kura lilianza Jumamosi katika uchaguzi wa kitaifa uliokuwa na ushindani mkali nchini Malaysia ambao utaamua iwapo muungano wake unaotawala kwa muda mrefu unaweza kurejea baada ya kushindwa vibaya miaka minne iliyopita.

Kambi ya mageuzi ya kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim inatabiriwa kuongoza, lakini huku kambi tatu kuu zikiwania kura, wachambuzi wanasema ni vigumu kutabiri matokeo na yanaweza kushuhudia miungano mipya ikiundwa ikiwa hakutakuwa na mshindi wa moja kwa moja.

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa kubwa kufikia saa kumi jioni saa za huko, huku asilimia 70 ya raia milioni 21.1 wa Malaysia waliostahili kupiga kura zao kwa wabunge 222 katika Bunge la shirikisho na wawakilishi katika mabunge matatu ya majimbo, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.

Upigaji kura wa viti viwili vya serikali kuu umeahirishwa baada ya kifo cha mgombea katika jimbo moja na hali mbaya ya hewa katika jimbo jingine. Matokeo yanatarajiwa baadaye leo Jumamosi. Takriban wapiga kura wapya milioni 6 tangu mwaka 2018 waliongeza hali ya sintofahamu katika kinyang'anyiro hicho kikali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG