Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:08

Raia wa Iran wanazidi kufanya maandamano yanayotikisa utawala wa nchi


Waandamanaji nchini Iran katika moja ya picha zilizochukuliwa hivi karibuni
Waandamanaji nchini Iran katika moja ya picha zilizochukuliwa hivi karibuni

Vuguvugu hilo lililodumu kwa takriban miezi mitatu lilichochewa na kifo cha Mahsa Amini ambaye alikuwa amekamatwa na polisi wa maadili wa Jamhuri ya Kiislamu. Inaleta changamoto kubwa kwa utawala wa Iran tangu kuondolewa madarakani kwa shah mwaka 1979.

Raia kadhaa wa Iran siku ya Jumapili walikuwa katika hatari ya kunyongwa kufuatia maandamano ambayo yameutikisa utawala wa kidini nchini humo, makundi ya kutetea haki za binadamu yameonya, baada ya upinzani wa kimataifa juu ya hatua ya Iran ya kumnyonga mtu mmoja mara ya kwanza kwa kuhusishwa na vuguvugu la waandamanaji.

Vuguvugu hilo lililodumu kwa takriban miezi mitatu lilichochewa na kifo cha Mahsa Amini, ambaye alikuwa amekamatwa na polisi wa maadili wa Jamhuri ya Kiislamu.

Inaleta changamoto kubwa kwa utawala huo tangu kuondolewa madarakani kwa shah mwaka 1979.

Iran inayaita maandamano hayo kuwa "ghasia" na inasema yametiwa moyo na maadui zake wa kigeni.

Mamlaka zinajibu kwa msako wa wanaharakati wanasema unalenga kuzua hofu kwa umma.

Iran siku ya Alhamisi ilimuua Mohsen Shekari, 23, ambaye alikuwa amekutwa na hatia ya kumshambulia mwanachama wa vikosi vya usalama. Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema mchakato wake wa kisheria, ambao waliuelezea kama kesi iliyoonyeshwa wazi, uligubikwa na uharaka usiostahili.

XS
SM
MD
LG